Jeshi la ulinzi wa mapinduzi la Iran leo limeanza luteka ya baharini katika mlango bahari wa Hormuz, kilomita karibu mia moja tu kutoka manuwari za nchi za magharibi, zinazohusika katika vita dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh lilipoegeshwa.
Vikosi vitatu vya jeshi la utawala wa Iran vinashiriki katika luteka hiyo ya kawaida ya kijeshi, nje ya kisiwa cha Qeshm na iliopewa jina la " Muhammad ni mtume mkuu ." Televisheni ya taifa imeonyesha shambulio la kombora la kisasa likifyatuliwa kutoka pwani. walinzi wa mapinduzi ndio wanaohusika na ulinzi wa majeshi katika ghuba. majeshi ya majini yanakadiriwa kuwa na karibu askari 20,000 wakiwa na jukumu la kuzingira mlango bahari wa Hormuz pindi Iran ikishambulia. Mlango bahari huo ndiko kunakopitia theluthi moja ya safari za meli zikiwemo zile za mafuta.
Luteka hiyo ya vikosi vya Iran inafanyika siku mbili baada ya manuwari ya Ufaransa ya kubebea ndege charles de Gaulle kuanza operesheni katika Ghuba, ikiwa ni sehemu ya muungano unaopambana na kundi la kigaidi la Daesh nchini Iraq na Syria.
Luteka hii ya kijeshi ni luteka ya pekee kufanywa na majeshi ya ulinzi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran, ambapo majeshi yameonyesha uwezo wake wa kijeshi wa hali ya juu, na kutoa ujumbe kwamba wako tayari kukabiliana na adui yeyote mwenye kuwa na mawazo potofu ya kuivamia jamhuri ya kiislamu ya Iran.
Iran ni nchi ya waajemi inayopakana na nchi za kiarabu, nchi za kiarabu zimepandikizwa chuki dhini ya Iran hivyo nchi nyingi za kiarabu kama Saudia Arabia zinaonyesha uadui wa dhahiri dhidi ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran. Iran ni nchi inayosifika kwa maendeleo ya katika nyanja mbalimbali ikiwemo sayansi na teknolojia na maendeleo katika sekta ya kijeshi na utengenezaji wa silaha za kisasa.



